Rais wa Ukraine Zelensky awasihi wanajeshi wa Urusi wasipigane

0

Zelensky amesema majeshi ya Urusi yatapata hasara kubwa wakati ambapo yanajiandaa kwa mashambulizi mapya katika eneo la mashariki la Donbas na alitoa wito kwa wanajeshi wa Urusi kuokoa maisha yao, akisema “afadhali kuishi Urusi kuliko kufa kwenye ardhi ya Ukraine.”

Rais wa Ukraine pia alizungumzia mashambulio ya anga ya siku ya Jumamosi ambapo uwanja wa ndege katika mji wa pwani wa Odesa uliharibiwa kwa makombora ya Urusi. Odesa ni mji ambao hapo awali ulikuwa kivutio maarufu cha watalii kutoka Urusi.

Gavana wa mkoa wa Odessa, Maxim Marchenko, amesema Urusi imeushambulia kwa makombora na kuuharibu uwanja huo na kuilenga miundombinu na mifumo ya ugavi ya mji huo wa magharibi mwa Ukraine.

Meya wa mji wa Odesa, Gennadiy Trukhanov, amesema imechukua miaka 10 kuujenga uwanja huo wa ndege, ambao ulifunguliwa rasmi mnamo Julai mwaka jana.

Taarifa zaidi zinafahamisha kuwa takriban raia 20, wakiwemo watoto kadhaa, wamefanikiwa kuondoka kutoka kwenye kiwanda cha chuma kilichopo katika mji wa bandari wa Mariupol nchini Ukraine.

Kikosi cha jeshi la Ukraine cha Azov, ambacho kimekuwa kikipambana kulikomboa eneo hilo, kimesema raia hao 20 wameondoka, na wameelekea katika mji wa Zaporizhzhia ulio umbali wa kilomita 225 kaskazini magharibi.

Haijafahamika wazi iwapo zoezi hilo la kuwahamisha watu liliongozwa na Umoja wa Mataifa na pia kama shughuli zaidi za kuwahamisha watu zitaendelea.

Leave A Reply

Your email address will not be published.