Rais wa Kenya, ametangaza kuongeza kima cha chini cha mshahara

0

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi leo ametangaza kuongeza kima cha chini cha mshahara wa Wafanyakazi kwa asilimia 12.

Rais Kenyatta amesema uamuzi wa kuongeza kima cha chini cha mshahara una lengo la kuongeza nguvu kazi ya nchi dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha kunakosababishwa na sababu kadhaa za kiuchumi za nje.

Kima cha chini cha mshahara Kenya kwa sasa ni Ksh. 13,500 ( Tsh. 271,089) ambacho kilifanyiwa mapitio kwa mara ya mwisho mwaka 2018.

Leave A Reply

Your email address will not be published.